Read the book: «Freddie Yule Mbweha Mjaja»
Freddie yule Mbweha Mjanja
Na Rotimi Ogunjobi
Aliyetafsiri ni Ephraim Kamau Njoroge
Kuelezea kwa uchoraji imefanyiwa na Ryan Ball
Mfululizo wa Vitabu vya Watoto na Auntie Mimie
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoruhusiwa kutumiwa au kunakiliwa vyovyote vile bila ruhusa ya mwandishi, isipokuwa tu kwa unakili wa kifupi ulioingizwa kwa uchapaji au kwa jarida muhimu
Utengaji
Kitabu hiki kimetengwa kwa watoto wote wanaohusika katika maisha yangu
Papa Leonardo alikuwa simba pekee kwa msitu. Lakini sasa alikuwa amazeeka na alijua ya kwamba, hivi karibuni ingekuwa vigumu sana kwake kwenda kuwinda ili apate chakula.
“Kama sitaweza kuwinda ili nipate chakula, nitakufa kwa jaa,” akahema kwa uchovu.
Lakini siku moja, alipata wazo la busara na kwa hivyo akawaita wanyama wengine wote pamoja akaongea na wao:
“Nawashukuru nyote kwa kuja na hii inaonyesha ya kwamba mnanipenda na kuniheshimu kama mfalme wenu. Nina hakika mlikuja kwa maana mimi si mfalme wa uovu.”
The free excerpt has ended.